Media Centre » Announcements

UTEUZI WA MKURUGENZI - MAMLAKA YA MAJISAFI NA USAFI WA MAZINGIRA MOSHI

Waziri wa Maji Mhe. Prof. Makame Mbarawa (Mb) amemteua Eng. Christopher Comer Shiganza kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mjini Moshi (MUWSA). Uteuzi huu utadumu kwa kipindi cha miaka minne.

Taarifa ya Katibu Mkuu, Wizara ya Maji Prof. Kitila Mkumbo imesema kuwa uteuzi wa Eng. Shiganza umeanza tarehe 16 Aprili, 2020 na umefanyika chini ya Sheria ya Huduma ya Maji na Usafi wa Mazingira Namba 5 ya mwaka 2019.

Kufuatia uteuzi huu Eng. Shiganza ambaye alikuwa Meneja Ufundi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Tabora (TUWASA), atakuwa Katibu wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira - Mjini Moshi (MUWSA).

Aidha, kwa hatua hii aliyekuwa akikaimu nafasi ya Mkurugenzi wa MUWSA Eng. Aron Joseph anarudi katika Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) alipokua awali kuendelea na majukumu yake ya kawaida.