Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Maji

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Moshi(muwsa)

MUWSA Logo
Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso asimamia utiaji wa saini mikataba ya utendaji kazi Sekta ya Maji
23 Jul, 2026
Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso asimamia utiaji wa saini mikataba ya utendaji kazi Sekta ya Maji

Waziri Aweso asimamia utiaji saini mikataba ya utendaji kazi sekta ya maji

Dodoma, Julai 22, 2026 – Waziri wa Maji, Jumaa Aweso, leo ameongoza zoezi la utiaji saini wa mikataba ya utendaji kazi kati ya Wizara ya Maji, Mamlaka za Majisafi na Usafi wa Mazingira pamoja na Bodi za Maji za Mabonde nchini.

Zoezi hilo linalenga kuimarisha uwajibikaji, kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma za maji na kuhakikisha Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Maji zinatekeleza majukumu yake kwa kuzingatia malengo na viwango vya utendaji vilivyowekwa.

Akizungumza katika hafla hiyo, Waziri Aweso alisisitiza umuhimu wa uwajibikaji na usimamizi madhubuti wa miradi ya maji ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora, salama na endelevu. 

Aidha, aliwataka viongozi wa Taasisi hizo kutekeleza majukumu yao kwa weledi na kuhakikisha mikataba hiyo inaleta matokeo chanya kwa wananchi.