Malalamiko ya Mteja

MAONI NA MALAMIKO YA WATEJA
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira AUWSA inapokea maoni na kushughulikia malalamiko kuhusu utoaji wa huduma. Mteja anaweza kuwasilisha malalamiko yake kwa kutumia njia zifuatazo:
- Kufika Ofisi za kanda za Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira zilizopo Mjini Kati, Njiapanda, Bomang'ombe, Mwika na Mkalama.
- Kuandika barua pepe kupitia (info@muwsa.go.tz ).
- Au kwa kupiga simu kupitia Kituo cha huduma kwa wateja kwa namba ya bure 0800110074 / 0800750386
- Namba ya WhatsApp 0739 100 207
UTARATIBU WA KUSHUGHULIKIA MALALAMIKO YA WATEJA
Malalamiko yote yatasikilizwa na kutatuliwa ndani ya siku 5 za kazi. Endapo mlalamikaji hataridhika na majibu yatakayotolewa na Mamlaka, anaweza kuwasilisha malalamiko yake kwa Mamlaka yaUdhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) kwa kufuata taratibu zilizoainishwa kwenye Sheria ya EWURA Sura 414, na Kanuni za EWURA za kuandaa na kuwasilisha malalamiko.
WASILISHA LALAMIKO LAKO KUPITIA:
Anuani: S.L.P 1001 MOSHI, KILIMANJARO, TANZANIA.
Simu ya huduma kwa wateja : 0800110074 / 0800750386 bure
Barua Pepe: info@muwsa.go.tz
Tovuti: www.muwsa.go.tz
WhatsApp: 0739 100 207
Simu ya Ofisi: +255 - 27 2751164
