Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Maji

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Moshi(muwsa)

MUWSA Logo
Miradi iliyokamilika

1.0 UTANGULIZI.

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Moshi (MUWSA) inazalisha jumla ya mita za ujazo 43,322 kwa siku sawa na asilimia 60 ya Mahitaji ya mita za ujazo 73,246. Upungufu wa Maji katika eneo la Manispaa ya Moshi ni mita za ujazo 17,593 kwa siku. Ili kukabiliana na changamoto ya upungufu wa maji kwa kutumia wataalamu wa ndani MUWSA iliamua kuanza kutekeleza Mradi wa upanuzi wa chanzo cha “Coffee curing” mnamo tarehe 25 Mei 2026 na unatarajia kukamilika tarehe 30 Juni 2027. Chanzo hiki kinatarajia kuongeza kiasi cha Maji yanayozalishwa kwa siku kutoka mita za ujazo 750 hadi 3,840 kwa siku.

Mradi huu unatekelezwa katika awamu mbili (Phase).

2.0 LENGO LA MRADI.

Lengo la kutekeleza mradi huu ni kuboresha hali ya upatikanaji wa huduma ya Majisafi na Salama katika maeneo ya Manispaa ya Moshi haswa katika Kata ya Kaloleni, Njoro na Miembeni zenye jumla ya wakazi wapatao 42,283.

  1. GHARAMA YA MRADI.

Mradi huu hadi kukamilika kwake utagharimu kiasi cha Tsh. 646,197,482.10. ambapo kwa awamu ya kwanza kiasi cha Sh. 70,037,850.00 na kwa awamu ya pili kiasi cha Sh. 576,159,632.10

  1. HATUA ZA UTEKELEZAJI WA MRADI.
    1. Awamu ya Kwanza.

Utekelezaji wa mradi kwa awamu ya kwanza umekamilika kwa asilimia 100 na kazi zifuatazo zimetekelezwa;

  1. Upanuzi wa chanzo.
  2. Ujenzi wa choo cha mtumishi.
    1. Awamu ya pili.

Utekelezaji wa mradi kwa awamu ya pili unatarajia kuanza mwezi Oktoba 2026 na kukamilika mwezi Juni 2027 kazi zifuatazo zimepangwa kutekelezwa;

  1. Uchimbaji wa mtaro na ulazaji wa bomba lenye kipenyo cha inchi 8 lenye urefu wa kilomita 6.
  1. MAFANIKIO YA MRADI.

Mradi huu utanufaisha wananchi wa Manispaa ya Moshi na maeneo mengine kwa kupata huduma bora na endelevu ya Majisafi na Salama.

  1. SHUKRANI.

Tunapenda kutoa Shukrani kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutuletea fedha za utekelezaji wa miradi kwa ajili ya kupunguza changamoto ya upungufu wa maji kwa Wananchi wa Wilaya ya Moshi.