Miradi inayoendelea
Mamlaka ilianza utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa chanzo cha maji cha Lyasongoro na Kyerio tarehe 13 Agosti 2024 na awamu ya kwanza ya mradi kukamilika tarehe 31 Machi, 2025. Ujenzi wa vyanzo hivi vinatarajiwa kuzalisha takribani lita 50 za maji kwa sekunde sawa na mita za ujazo 4,320 kwa siku. Mradi huu unatekelezwa katika awamu kuu mbili (phase) na unatekelezwa kwa kutumia fedha kutoka mapato ya ndani ya Mamlaka. Utekelezaji kwa awamu ya kwanza iliyohusu ujenzi wa vyanzo imekamilika.
- LENGO LA MRADI
Lengo la kutekeleza mradi huu ni kuboresha hali ya upatikanaji wa huduma ya Majisafi na Salama katika Kata ya Marangu Mashariki na unatarajiwa kunufaisha wakazi wapatao 10,574 katika vijiji vya Samanga, Rauya, Mshiri na Ashira.
- GHARAMA YA MRADI
Mradi huu hadi kukamilika kwake utagharimu kiasi cha Tsh. 1,470,121,709.10. ambapo kwa awamu ya kwanza kiasi cha Tsh. 281,052,072.85 kilitumika na kwa awamu ya pili kiasi cha Tsh. 1,189,069,636.25 kinatarajia kutumika.
- HATUA ZA UTEKELEZAJI WA MRADI.
- AWAMU YA KWANZA
Utekelezaji wa mradi kwa awamu ya kwanza ulianza 13 Agosti, 2024 na kukamilika kwa asilimia 100. Kazi zifuatazo zimetekelezwa na kukamilika;
- Ujenzi wa chanzo cha Lyasongoro pamoja na Kyerio.
- Ujenzi wa kituo cha kukusanya maji (Collection Chamber) moja (1).
- Uchimbaji na ulazaji wa bomba kilomita 2 kutoka kwenye chanzo hadi kwenye Collection Chamber.
- Ujenzi wa fensi (uzio) katika vyanzo vyote.
- AWAMU YA PILI
Utekelezaji wa mradi awamu ya pili umeanza tarehe 03/08/2026 na unatarajia kukamilika tarehe 30/11/2026.Kazi zinazotekelezwa ni pamoja na uchimbaji wa mtaro na ulazaji wa bomba lenye kipenyo cha inchi 8 na 6 lenye urefu wa kilomita 13.Mradi umefikia asilimia 53.7
- Mamlaka imepata kibali cha Ununuzi wa bomba za urefu wa kilomita 13.
- Uchimbaji wa mtaro unaendelea ambapo hadi sasa urefu wa kilomita 8 umefikia asilimia 61.5
- Jumla ya urefu wa kilomita 4.6 zimechibwa na kulazwa bomba, kazi hii inaendelea imefikia asilimia 46
- MAFANIKIO YA MRADI.
Kutekelezwa kwa mradi huu kutasaidia kuondoa changamoto ya majisafi na salama katika kata ya Marangu Mashariki, Aidha Mamlaka inatoa shukrani kwa viongozi wa kata ya Marangu Mashariki pamoja na wananchi wote kwa ushirikiano wote wanaotuonesha wakati wa utekelezaji wa mradi huu.
- SHUKRANI.
Tunapenda kutoa shukrani kwa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutuletea fedha za utekelezaji wa mradi huu kwa ajili ya kupunguza changamoto ya upungufu wa maji kwa wananchi wa Kata ya Marangu Mashariki.
