MUWSA YAKAMILISHA UTEKELEZAJI WA MAELEKEZO YA MHE: DKT: MWIGULU LAMECK NCHEMBA KWENYE KATA YA MABOGINI
10 Mar, 2026
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Moshi imekamilisha utekelezaji wa maelekezo ya Mhe. Waziri Mkuu, Dk Mwigulu Nchemba ya kuhakikisha wananachi wanapata huduma ya majisafi na salama katika kitongoji cha Uru kilichopo kijiji cha Chekereni kwenye Kata ya Mabogini.
Dkt. Mwigulu alitoa maelekezo hayo akiwa kwenye ziara ya kikazi Mkoani Kilimanjaro.
Aidha, wananchi wa kitongoji hicho wameishukuru Serikali ya awamu ya sita kwa namna inavyotekeleza kazi zake kwa vitendo.
