Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Maji

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Moshi(muwsa)

MUWSA Logo
SERIKALI KUPITIA WIZARA YA MAJI IMEAZIMIA KUTATUA CHANGAMOTO ZA UPATIKANAJI WA HUDUMA YA MAJISAFI KWENYE KATA ZA URU MASHARIKI PAMOJA NA KIMOCHI
17 Jul, 2026
SERIKALI  KUPITIA WIZARA YA MAJI IMEAZIMIA KUTATUA CHANGAMOTO ZA UPATIKANAJI WA HUDUMA YA MAJISAFI KWENYE KATA ZA URU MASHARIKI PAMOJA NA KIMOCHI

Serikali kupitia Wizara ya Maji imeazimia kutatua changamoto za upatikanaji wa huduma ya majisafi  kwenye Kata za Uru Mashariki pamoja na Kimochi kwa kutekeleza miradi ya maji yenye thamani ya Tshs: 754,996,141.04


Katika Kata ya Uru Mashariki, Mamlaka itafanya ukarabati wa vyanzo vya Kirikuna pamoja na Ochai vinavyokwenda kuzalisha jumla ya mita za ujazo 800 kwa siku.

Sambamba na ukarabati, Mamlaka pia italaza bomba zenye vipenyo mbalimbali urefu wa kilomita 9.9.

Aidha, kwenye Kata ya Kimochi Mamlaka itatekeleza mradi wa kulaza bomba urefu wa kilomita 28.7 kwenye  vijiji vya Shia, Kisaseni pamoja na Mdawi.

Mamlaka imewasilisha taarifa hiyo kwenye kikao cha pamoja baina ya  viongozi wa Chama pamoja na  Serikali kwa kushirikiana na Ofisi ya Mbunge wa  Jimbo la Moshi Vijijini.