MUWSA yapanda Miti 500 Kuadhimisha Wiki ya Maji Moshi
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Moshi, MUWSA, imepanda zaidi ya miti 500 katika Shule ya Sekondari Njia Panda, iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Moshi, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Maji nchini.
Akizungumza katika zoezi hilo leo Alhamisi Machi 19, 2026, kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Afisa Mazingira Peter Atundu amesema hatua hiyo inalenga kuunga mkono juhudi za Rais Samia Suluhu Hassan katika utunzaji wa mazingira.
Kwa upande wake, Meneja wa Maji Safi na Usafi wa Mazingira kutoka MUWSA, Mhandisi Philbert Boniface, amesema upandaji wa miti hiyo unalenga kuimarisha mazingira na kulinda vyanzo vya maji kwa manufaa ya jamii yote.
Wadau walioshiriki zoezi hilo wamehimizwa kuendelea kupanda miti kwa wingi, wakisisitiza kuwa miti ni chanzo muhimu cha uhifadhi wa maji na mazingira kwa ujumla.
