MUWSA YATWAA TUZO YA MAMLAKA BORA YA UTOAJI WA HUDUMA YA MAJISAFI NA USAFI WA MAZINGIRA KWA MWAKA WA FEDHA 2024/25
19 Mar, 2026
Kwa Mara nyingine tena, Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Moshi ( MUWSA) imeendelea kutwaa tuzo mbalimbali za EWURA ambapo kwa mwaka wa fedha 2024/25 imeibuka mshindi wa kwanza katika utoaji wa huduma za majisafi na usafi wa mazingira kwenye kundi la mamlaka zinazohudumia zaidi ya wateja 20,000.

Tuzo hizi zitaendelea kuwa chachu ya kuwajibika vyema kwa wateja wetu ili kuhakikisha malengo ya Serikali na matarajio ya wananchi yanafikiwa kwa viwango vya juu.
MUWSA: Uwajibikaji na Huduma Bora Endelevu
