MUWSA YATOA KITITA CHA MILIONI MBILI KWA MWANANCHI ATAKAYETOA TAARIFA YA WIZI WA MITA ZA MAJI
MOSHI
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Moshi imetangaza dau nono la Tshs: milioni mbili (2,000,000) kwa mwananchi yeyote atakayeleta taarifa za kuthibitika za wananchi wasio waaminifu wanaohujumu miundombinu ya maji kwenye maeneo ya Mamlaka.
Dau hili nono limetokana na kushamiri kwa vitendo vya wizi wa mita za maji pamoja na viungio vyake, mifuniko ya chemba za maji pamoja na gate valve.
Takribani mita 266 zimeibiwa kuanzia mwezi Januari - Machi 2026 kwenye Kata za Makuyuni, Njiapanda, Majengo, Mwika kaskazini pamoja na maeneo jirani na hivyo kuisababishia Serikali kupata hasara ya zaidi ya Tsh; 37,240,000
Aidha, Mamlaka inawahakikishia wananchi taarifa watakazozitoa zitafanyiwa kazi kwa USIRI mkubwa kwa lengo la kutokomeza changamoto hii ya hujuma za miundombinu.
Aidha, Mamlaka imetoa namba ya simu ambayo ni 0791992525 na kuwa namba hiyo ni kwa ajili ya kuwasilisha taarifa hizo za hujuma
