Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Maji

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Moshi(muwsa)

MUWSA Logo
MWENGE WA UHURU WATEMBELEA NA KUWEKA JIWE LA MSINGI UBORESHAJI NA UPANUZI WA CHANZO CHA CHEMCHEMI YA COFFEE CURING.
06 Jul, 2026
MWENGE WA UHURU WATEMBELEA NA KUWEKA JIWE LA MSINGI UBORESHAJI NA UPANUZI WA CHANZO CHA CHEMCHEMI YA COFFEE CURING.

Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa zimeridhishwa na utekelezaji wa Mradi wa Upanuzi na Uboreshaji wa Chanzo cha maji Coffee Curing unaotekelezwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Moshi(MUWSA)

Hayo yamesemwa na kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa Ndugu: Wazo  Michael  Mwang'onda wakati alipofika katika Chanzo hicho kwa ajili ya kufanya ukaguzi na hatimae kuridhia kuweka Jiwe la Msingi.

Licha ya kufurahishwa na utekelezaji wa mradi huo unaosimamiwa na wataalam wa ndani, Ndugu Mwang"onda amewataka wananchi kutunza vyanzo vy maji kwa faida ya sasa na vizazi vijavyo.

Kiongozi huyo pia ameendelea kuishukuru Serikali ya Awamu ya sita inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuleta fedha za miradi mizuri ya maji inayolenga kumtua Mama ndoo kichwani