WIKI YA HUDUMA KWA MTEJA
Katika kuadhimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja mwaka 2026 yenye kauli mbiu ya "The Extra Mile" - Hatua Zaidi, Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Moshi (MUWSA) imetekeleza kauli hiyo kwa vitendo kwa kufanya hamasa ya utunzaji wa mazingira katika Kata ya Njiapanda.

_1791550680.jpeg)
MUWSA imewafikia wanafunzi na walimu wa Shule za Msingi Corona, Darajani, na Njiapanda na kutoa miche takribani miche 300 ya matunda na kivuli pamoja na vifaa vya kuhifadhia taka.

Akizungumza wakati wa kabidhi hiyo, Meneja wa Huduma kwa Wateja, Mwandani Mtony, amesisitiza kuwa huduma bora ya maji inapaswa kwenda sambamba na uhifadhi wa mazingira salama kwa jamii.
_1791550745.jpeg)
Uongozi na wanafunzi wa shule hizo wametoa shukrani zao na kuahidi kuitunza miche hiyo pamoja na kutumia vifaa vya taka ipasavyo ili kuboresha mandhari na usafi wa shule zao.
MUWSA inaendelea kujitolea kwenda hatua zaidi ya matarajio ya wateja wake ili kujenga mazingira safi na endelevu kwa kizazi cha leo na kesho.

