Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Maji

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Moshi(muwsa)

MUWSA Logo
MUWSA YAWATUNUKU WATEJA VINARA WA UTOAJI TAARIFA ZA MIVUJO YA MAJI
09 Oct, 2026
MUWSA YAWATUNUKU WATEJA VINARA WA UTOAJI TAARIFA ZA MIVUJO YA MAJI

Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Moshi (MUWSA), _Mhandisi Kija Limbe, leo amefungua rasmi _Wiki ya Huduma kwa Mteja yenye kauli mbiu ya "Hatua Moja Zaidi (Extra Mile)".

Katika ufunguzi huo, Mhandisi Limbe ametumia nafasi hiyo kuwatunuku zawadi baadhi ya _wateja vinara_ wanaojitokeza kwa kutoa taarifa za mivujo ya maji na ukosefu wa huduma katika maeneo mbalimbali ya huduma ya Mamlaka.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Mhandisi Kija amesema Mamlaka inathamini mchango mkubwa wa wateja hao ambao wamekuwa kiungo muhimu kati ya Mamlaka na jamii.

"Wapo wateja wengi wanaotoa taarifa mbalimbali za changamoto za huduma, na hawa tuliowatunuku leo ni wawakilishi tu wa wateja wote wa Mamlaka. Tunawashukuru sana," alisema Mhandisi Kija.