MHANDISI KUNDO MATHEW (Mb) NAIBU WAZIRI WA MAJI AZINDUA BODI YA TISA YA WAKURUGENZI WA MAMLAKA YA MAMLAKA YA MAJISAFI NA USAFI WA MAZINGIRA MOSHI (MUWSA)
Mhandisi Kundo Mathew(Mb), Naibu Waziri wa Maji amezindua Bodi ya Tisa ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Moshi (MUWSA) huku akiisisitizia kuhakikisha huduma ya maji inapatikana kwa uhakika.
Sambamba na hilo Mha: Kundo amesisitiza kuwa, dhamana hiyo si heshima pekee, bali ni wito wa kulitumikia Taifa na kuhakikisha maji, ambayo ni uhai, afya na msingi wa maendeleo, yanapatikana kwa Wananchi kwa uhakika.

Aidha, amesisitiza juu ya kudhibiti maji yanayopotea ili rasilimali hii adhimu iweze kunufaisha Umma kwa ukubwa zaidi.
Mafanikio ya Taasisi hayajengwi na mtu mmoja au bodi moja, hivyo nawaasa wajumbe wapya wa Bodi ya Tisa inapaswa kuendeleza mazuri yaliyoachwa na Bodi ya Nane, kuyaboresha na kuongeza kasi katika maeneo yenye changamoto.

