Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Jiji la Arusha (MUWSA) inatumia mfumo wa malipo wa kielektroniki wa Serikali (Government Elektronic Payment Gateway system – (GePGS). Kwenye Mfumo huu,mteja tafanya malipo ya Ankara ya maji kwa kutumia kumbukumbu namba yenye tarakimu 12 atakayotumiwa kila mwezi katika Ankara yake na siyo akaunti namba kama ilivyozoeleka. Wakati wa kufanya malipo, hatua zifuatazo zitatumika kutegemeana na mtandao.
Tigo-Pesa
Piga *150*01#
Bonyeza 4 Kulipia bili
Bonyeza 5 Malipo ya Serikali
Ingiza namba ya Malipo (Control Number, Mfano 991631XXXXXX)
Weka Kiasi
Ingiza Namba ya Siri
Bonyeza 1 Kuthibitisha
M-pesa, Piga
Piga *150*00#
Chagua 4 –Lipa kwa M-Pesa
Chagua 5 – Malipo ya Serikali
Chagua 1 Namba ya Malipo
Ingiza 1 Namba ya Malipo
Ingiza namba ya Malipo (Control Number Mfano: 991631XXXXXX)
Weka Kiasi
Ingiza Namba ya Siri
Bonyeza 1 Kuthibitisha
TTCL PESA
Piga *150*71#
Chagua 5 – Lipia Bili
Chagua 3 – Malipo ya Serikali
Ingiza kumbukumbu namba (Control Number inayoanza na 991631XXXXXX)
Ingiza kiasi
Ingiza namba ya siri
BENKI
Njia nyingine ni kutumia benki za CRDB, NMB na Wakala zake za FAHARI HUDUMA na NMB Wakala> Mteja atapaswa kufika katika benki husika na kuonesha kumbukumbu namba ya malipo ya Ankara aliyotumiwa na Mamlaka, na ndipo Afisa wa benki atamwelekeza jinsi ya kufanya malipo hayo.