Customer Services

New Connections

HUDUMA ZITOLEWAZO NA MAMLAKA

Mamlaka inatoa huduma kuu mbili; Huduma ya Usambazaji Majisafi na Huduma ya Uondoaji Majitaka.  Zaidi ya huduma tajwa hapo juu Mamlaka pia inatoa huduma ya ushauri wa kitaalamu katika huduma hizo mbili ambazo imepewa jukumu la kisheria kuzisimamia. 

Ili kuunganishiwa huduma ya majisafi, mteja yeyote wa Mamlaka atapaswa kukamilisha hatua zifuatazo

 1. Kujaza fomu ya maombi ya kuunganishwa kwenye huduma ya majisafi. Huduma hii inapatikana katika ofisi za Mamlaka.
 2. Kwa maeneo yaliyopimwa, mwombaji wa huduma hiyo lazima aje na nyaraka halali za uthibitisho wa umiliki wa eneo linalohitaji kuunganishiwa huduma ikiwemo mkataba wa mauzo ya kiwanja au hati ya nyumba/kiwanja.
 3. Kwa maeneo ambayo hayajapimwa mwombaji atapaswa kupata barua ya utambulisho kutoka kwa Mwenyekiti wa Mtaa na kuthibitishwa na Afisa Mtendaji wa Mtaa/Afisa Mtendaji wa Kata ikiwa mwombaji ni mkazi wa eneo la manispaa ya Moshi, au apate utambulisho kutoka kwa Mwenyekiti wa Kitongoji/Kijiji na kuthibitishwa na Afisa Mtendaji wa Kijiji ikiwa mwombaji ni mkazi wa eneo la Halmashauri za Wilaya.
 4. Mteja atafanyiwa “survey” ndani ya siku tatu (3) za kazi baada ya fomu ya maombi kukamilika na kujulishwa gharama za maunganisho mapya anazopaswa kulipa.
 5. Mteja ataunganishiwa huduma ya majisafi ndani ya siku saba (7) za kazi baada ya malipo kukamilika.
 6. Mamlaka haitapokea fedha kwa ajili ya maunganisho mapya endapo kutajitokeza tatizo la kutokuwepo kwa vifaa vya maunganisho.
 7. Endapo mteja atakuwa tayari kulipia gharama za kuunganishiwa huduma wakati amepewa taarifa ya kutokuwepo kwa vifaa vya maunganisho, hivyo atatakiwa kukubali kwa maandishi kusubiri vifaa pasipo kudai fidia kwenye Mamlaka.

Ili kudhibiti ubora wa vifaa, gharama ya kuunganisha huduma ya majisafi inajumuisha ununuzi wa vifaa kutoka Mamlaka pamoja na ada ya kuunganisha maji (New water connection fee). 

Ili kuunganishiwa huduma ya majitaka, mkazi yeyote wa Mji wa Moshi atapaswa kukamilisha hatua zifuatazo:

 1. Kujaza fomu ya maombi ya kuunganishwa kwenye huduma ya majitaka. Huduma hii inapatikana katika ofisi za Mamlaka. 
 2. Kwa maeneo yaliyopimwa, mwombaji wa huduma hiyo lazima aje na nyaraka halali za uthibitisho wa umiliki wa eneo linalohitaji kuunganishiwa huduma ikiwemo mkataba wa mauzo ya kiwanja au hati ya nyumba/kiwanja. 
 3. Kwa maeneo ambayo hayajapimwa mwombaji atapaswa kupata barua ya utambulisho kutoka kwa Mwenyekiti wa Mtaa na kuthibitishwa na Afisa Mtendaji wa Mtaa/Afisa Mtendaji wa Kata ikiwa mwombaji ni mkazi wa eneo la manispaa ya Moshi, au apate utambulisho kutoka kwa Mwenyekiti wa Kitongoji/Kijiji na kuthibitishwa na Afisa Mtendaji wa Kijiji ikiwa mwombaji ni mkazi wa eneo la Halmashauri za Wilaya.
 4. Mteja atafanyiwa “survey” ndani ya siku tatu (3) za kazi baada ya fomu ya maombi kukamilika na kujulishwa gharama za maunganisho mapya anazopaswa kulipa.
 5. Mteja ataunganishiwa huduma ya majitaka ndani ya siku saba (7) za kazi baada ya malipo kukamilika.
 6. Mamlaka haitapokea fedha kwa ajili ya maunganisho mapya endapo kutajitokeza tatizo la kutokuwepo kwa vifaa vya maunganisho.
 7. Endapo mteja atakuwa tayari kulipia gharama za kuunganishiwa huduma wakati amepewa taarifa ya kutokuwepo kwa vifaa vya maunganisho, hivyo atatakiwa kukubali kwa maandishi kusubiri vifaa pasipo kudai fidia kwenye Mamlaka.

Ili kuhakikisha ubora wa huduma, gharama za kuunganishiwa huduma ya majitaka inajumuisha bomba, viungio na vifaa vingine vyote kutoka Mamlaka tu, pamoja na ada ya kuunganisha huduma ya majitaka (new sewerage connection fee).