Mamlaka imefanya semina kwa viongozi wa Kata pamoja na Maafisa Tarafa lengo likiwa ni muendelezo wa mashirikiano ya pamoja baina ya Mamlaka na wadau wake.
Kufuatia mashirikiano hayo Mamlaka imeandaa semina ya mapitio ya Mkataba wa Huduma kwa Mteja ambapo kupitia mkataba huo wamepata elimu ya kujua haki na wajibu wa wateja kwa Mamlaka lakin pia haki na wajibu wa Mamlaka kwa wateja wake.
Mamlaka itaendelea kushirikisha wadau wake lengo likiwa ni kuwa na uelewa wa pamoja na hivyo kusaidia utekelezaji wa shughuli zake ktk maeneo inayoyahudumia.