Media Centre » News and Events

Dawati La Habari La MUWSA Leo Machi 21, 2023

Habari za wakati huu mpenzi mtazamaji wa dawati la habari kutoka Mamlaka ya Maji Safi na Usafi Wa Mazingira Moshi MUWSA na nikukaribishe katika wasaa huu kupata machache yaliyojiri katika Mamlake yetu wiki hii.

Waziri wa Maji Mheshimiwa Jumaa Aweso amezindua bodi ya nane ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Moshi MUWSA.

Uzinduzi huu Umetanguliwa na Ziara ya Ukaguzi Wa Mradi wa Maji wa Same-Mwanga-Korogwe unaotekelezwa na serikali.

Awali Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mheshimiwa Nurdin Babu alitaka MUWSA kutosita kusitisha huduma kwa wadaiwa sugu wa madeni ya Maji.

Naye Mwenyekiti wa Bodi Mpya Prof. Jafari Kideghesho ambaye pia ni Mkuu wa Chuo cha Usimamizi Wanyamapori Mweka alipata fursa ya kutoa mwelekeo mpya wa bodi yake.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa MUWSA Mhandisi Kija Limbe alitoa Taarifa ya Uteklezaji wa shughuli za Mamlaka.

Kwa Taarifa zaidi na kupata habari nzima tafadhali Tembelea Kurasa zetu za Mitandao ya kijamii

Instagram: @muwsa_moshi. YouTube: MajiMoshi, Twitter: MajiMoshi