Media Centre » News and Events

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mjini Moshi yapanda kutoka Daraja A kwenda daraja AA

Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) amezindua Bodi 25 mpya za Mamlaka za Maji Nchini na kuwataka viongozi wa Sekta ya Maji kuhakikisha wanashirikiana na wadau pamoja na jamii inayowazunguka katika kuhakikisha Sekta ya Maji inasonga mbele. Kikao hicho kilichowakutanisha Bodi za Wakurugenzi pamoja na Menejimenti za Sekta ya Maji amesisitiza juu ya viongozi kutozoea changamoto za wananchi na hivyo kila Taasisi iweke mifumo na taratibu nzuri za kutatua changamoto za wateja. Aidha,Mhe. Aweso amemtaka Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Prof. Jamal Katundu kuhakikisha bodi hizo zinakuwa mkono wa wizara na kupokea maoni mbalimbali kutoa majibu kutoka kwa makundi mbalimbali wakiwemo viongozi wa kisiasa, Serikali, wafanyabiashara na wadau kwa ujumla. Sambamba na hilo,Mhe. Aweso ametunuku vyeti Mamlaka mbalimbali zilizohama Daraja ikiwa ni pamoja na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mjini Moshi ambayo imehama kutoka Daraja A kwenda daraja AA