Media Centre » News and Events

MUWSA MSHINDI WA PILI TUZO ZA EWURA MWAKA WA FEDHA 2022/2023

Ikiwa ni katika Maadhimisho ya Wiki ya Maji na mwaka huu ikibeba kaulimbiu:  Uhakika wa Maji kwa Amani na Utulivu ambapo Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati ikizindua rasmi Taarifa ya Utendaji kazi wa Mamlaka za Majisafi na Usafi wa Mazingira kwa mwaka wa fedha 2022/2023.

Katika Uzinduzi huo uliombatana na utoaji wa tuzo kwa Mamlaka zilizofanya vizuri zaidi katika makundi mbalimbali na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Moshi ikiibuka mshindi wa pili katika kundi la Usambazaji Majisafi na Usafi wa Mazingira  ikishindanishwa na Mamlaka nyingine 19 zenye zaidi ya wateja elfu 20,000.

Akizungumza na watendaji wa Sekta ya Maji Nchini Mhandisi: Mwajuma Waziri  Katibu Mkuu Wizara ya Maji ambaye pia alikuwa Mgeni rasmi amesema, " Nazipongeza sana Mamlaka zilizopokea tuzo siku ya leo nakuzitaka Mamlaka ambazo hazijafanya vizuri kujitathimini"

Uzinduzi huo ulihudhuriwa pia na Wenyeviti wa Bodi wa Mamlaka, Menejimenti pamoja na viongozi mbalimbali wa Wizara ya Maji.