Media Centre » News and Events

MUWSA YANG’ARA TUZO ZA NBAA

Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi (NBAA) imeitunuku MUWSA Tuzo ya Uandaaji Bora wa taarifa za kifedha yaani Best Presented Financial Statements kwa mwaka 2021/22.

Tuzo hii imetolewa kwa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Moshi(MUWSA) ikiwa imeshindanishwa na Mamlaka zote za Maji Tanzania na Mamlaka hiyo kuibuka mshindi wa kwanza.

Tuzo hii imekabidhiwa tarehe 01 Dec 2023 Jijini Dar es Salaam.