Maji Cup League 2022.
Ligi ya Maji inaendelea kutimua vumbi kwa Kanda ya kaskazini ambapo asubuhi ya Leo Mkurugenzi Mkuu wa ATAWAS ambaye pia ndio mratibu mkuu wa mashindano haya akiwa katika picha na baadhi ya viongozi wakikagua vikosi vinavyoshuka dimbani Leo hii katika kiwanja Cha Njoro Wilayani Moshi.
Timu zinazoshuka dimbani ni kati ya Mamlaka ya Maji Moshi dhidi ya Kikosi kutoka Bodi ya Maji Bonde la Mto pangani lakini pia kwa upande wa netball ni kikosi kutoka Moshi Wssa dhidi ya Njoro United.
"Thamani ya Maji kwa Uhai na Maendeleo"