Ikiwa ni ziara ya mafunzo ya siku mbili ya Watumishi kutoka Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Iringa(IRUWASA) kwenye ofisi za Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Moshi(MUWSA),lengo ikiwa ni kubadilishana uzoefu wa shughuli mbalimbali zinazotekelezwa na Mamlaka hizo katika maswala ya Huduma kwa wateja, Utekelezaji wa miradi mbambali inayofanywa na wataalam wa ndani pamoja na mita za malipo ya kabla (Prepaid Water Meters).
Katika ziara hiyo watumishi hao wamepata wasaha wakutembelea vyanzo mbalimbali vya maji pamoja Mabwawa ya Majitaka katika eneo la Mabogini