Media Centre » News and Events

Watumishi wa MUWSA washiriki maadhimisho ya siku ya Saratani duniani

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Moshi yashiriki katika maadhimisho ya siku ya saratani duniani na katika Mkoa wa Kilimanjaro maadhimisho hayo yamefanyika katika  Hospitali ya Rufaa ya KCMC.

Aidha, katika maadhimisho hayo watumishi wa Mamlaka walipatiwa elimu juu yadalili za magonjwa ya saratani na njia mbalimbali za kujikinga na magonjwa ya saratani ikiwa ni pamoja na kufanya mazoezi na kujenga  utaratibu wa kujipima mara kwa mara.

Sambamba na hilo watumishi hao walipata nafasi ya kupima magonjwa mbalimbali kama vile sukari, pressure, HIV/AIDS pamoja na macho.

Mamlaka imekuwa na mashirikiano ya pamoja na Taasisi za afya zilizopo katika Mkoa wa Kilimanjaro  ili  kuhakikisha kwamba, afya za watumishi wake zinakua  njema wakati wote.

                *Maji kwa Afya*