Media Centre » News and Events

ZIARA YA KIKAZI NA KAMATI YA MAENDELEO KUKAGUA UTEKELEZAJI WA MRADI WA MAJISAFI MIWALENI

Ziara ya kikazi na kamati ya maendeleo ya kata ya njia panda imetembelea na kukagua utekelezaji wa mradi wa majisafi Miwaleni - njia panda, mradi wenye thamani ya Bilioni 2.3 unaotarajiwa kukamilika ifikapo mwezi September 2022.

Ziara hiyo iliyohusisha viongozi wa maendeleo ya kata ya njia panda ikiwemo Diwani Mhe. Lovness Mfinanga na wenyeviti wa vitongoji walipata bahati ya kukutana na Mhandisi Kija Limbe, Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na usafi wa Mazingira Moshi (MUWSA).

Mhandisi Kija Limbe amewahakikishia mradi wa majisafi wa Miwaleni - Njiapanda unaenda kufuta tatizo la majisafi kwa wakazi wa njiapanda, aidha amewaomba viongozi kuwa na subiria wakati wa kipindi Cha mpito na ameahidi pindi mabomba yatakapokuwa yamefika kipaumbele Cha ajira kitakuwa kwa wananchi wa njiapanda hivyo wajitokeze kwa wingi.

Kwa upande wake Kaimu Meneja Ufundi amesema mradi huo unajumuisha ujenzi wa (collection chamber), ujenzi wa ofisi katika chanzo Cha miwaleni, kituo Cha kukusanya na kusukuma maji Miwaleni, ulazaji wa Bomba kutoka miwaleni mpaka kituo Cha kusukuma maji Cha mabungo, Kisha ulazaji wa mabomba yatakayopeleka maji katika tenki la pofo. Aidha Muwsa itafanya uboreshaji wa miundombinu inayotumika kwa Sasa

Pia amezitaka taasisi zilizopo eneo la njiapanda zitapewa kipaumbele na kuwekewa laini yao maalumu.