Media Centre » News and Events

Ziara ya Mhe.Mbunge pamoja na Madiwani wa Manispaa ya Moshi katika Ofisi za MUWSA

Mbunge wa Manispaa ya Moshi Mhe. Priscus Tarimo akiwa ameambatana na madiwani wa Manispaa ya Moshi wamefanya ziara kwenye Ofisi za Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Moshi.

Ziara hiyo iliyolenga kuwapa elimu pamoja na kuwafahamisha shughuli mbalimbali zanazotekelezwa na Mamlaka ikiwa ni pamoja na miradi inayotekelezwa kupitia wataalam wa ndani.

Viongozi hao walipokea taarifa ya Utekelezaji wa shughuli za Mamlaka pamoja na kutembelea mradi wa majisafi wa Karanga " Darajani unaolenga kutatua changamoto ya upatikanji wa huduma kwenye maeneo ya Shabaha, Bomambuzi, Pasua pamoja na Mabogini.